December 04, 2017

BANDARI YA MBAMBABAY ITAKUZA UCHUMI

NA MWANDISHI WETU, SONGEA

NAIBU Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Mànyanya ameshauri kupanuliwa kwa bandari ya Mbamba Bay iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma ili kufungua milango ya uwekezaji katika ukanda wa kusini.





Mhandisi Manyanya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa, mkoani hapa alizungumza hayo katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Ruvuma, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea wiki iliyopita.

Naibu waziri huyo amesema bandari ya Mbamba Bay ikipanuliwa itatumika na nchi tatu za Tanzania, Malawi na Msumbiji hali ambayo itakuza uchumi na biashara hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya uchumi wa viwanda.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako